pmbet

Coastal na Singida kuwakilisha ligi kuu Kagame Cup

Sisti Herman

July 3, 2024
Share :

Droo ya makundi ya Kombe la klabu Bingwa Afrika mashariki na kati (CECAFA Kagame Cup) imechezeshwa leo ambapo ligi kuu Tanzania bara itawakilishwa na timu mbili, Singida Black Stars na Coastal Union baada ya Simba, Yanga na Azam kujiengua kwasababu ya ratiba.

Coastal Union ambao walimaliza nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ambao pia ni wawakilishi wa Tanzania kwenye kombe la shirikisho Afrika wapo kundi A wakiwa na timu za Al Wahdi ya Sudan, JKU ya Zanzibar na Dekedaha ya Somalia.

Singida Black Stars ambao walimaliza nafasi ya 7 kwenye ligi kuu Tanzania bara wakifahamika kama Ihefu wapo kundi C wakiwa na timu za El Merrikh ya Sudan, APR ya Rwanda na SC Villa ya Uganda.

Kundi lingine kwenye michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Julai 9 ni kundi B ambalo lina timu za Al Hilal ya Sudan, Gor Mahia ya Kenya, Red Arrows ya Zambia na Telecom ya Djibout.

Michuano hiyo itachezwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi na KMC Mwenge.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet