Coastal Union yagawa dozi ya mabao 2-0 kwa Mbeya City.
Joyce Shedrack
May 13, 2026
Share :
Klabu ya Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini dhidi Mbeya City na kufanikiwa kuvuna alama zote tatu.

Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City kuwa katika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 21 huku Coastal ikiwa nafasi ya 10 kwa pointi 25 japo pia haipo kwenye nafasi nzuri pia.
Mabao ya Coastal yamefungwa na Maabad Maabad 35’ kwa mkwaju wa penalti, na Saad Mwanza akikandamiza msumari wa pili dakika ya 74.





