Cole Palmer avunja ukimya kuhusu kuhamia Man U
Eric Buyanza
April 18, 2026
Share :

Mchezaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Cole Palmer amekanusha uvumi unaodai kuwa ataondoka kwenda Manchester United msimu huu wa joto.
Katika siku za karibuni kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu mchezaji huyo kutaka kuondoka Stamford.
Palmer mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na Chelsea mwaka 2023 kwa uhamisho wa pauni milioni 40 kutoka Manchester City.
Akizungumza na gazeti la The Guardian la nchini Uingereza alisisitiza kwamba hana mpango wa kuchomoka na atabaki Chelsea.
Palmer ana matumaini makubwa kwamba Chelsea inaweza kupambania "mataji makubwa" msimu ujao ikiwa wachezaji wa uhakika watasajiliwa.
Chelsea kwa sasa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza ikiwa pointi nne nyuma ya Liverpool.





