pmbet

Colombia,Iran na Panama zina wachezaji wenye umri mkubwa zaidi Kombe la Dunia.

Joyce Shedrack

June 6, 2026
Share :

Timu ya taifa ya Panama ndiyo inayoongoza kwa kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa zaidi katika Kombe la Dunia la 2026, ikiwa na wastani wa umri wa miaka 30.00 Inafuatiwa kwa karibu na Iran (miaka 29.81) na Colombia miaka 29.58.

Iran players granted visas from US to partake in World Cup | Flashscore.com

Wachezaji wenye umri mkubwa zaidi kwenye tiimu ya Panama ni Luis Mejía (Mlinda Lango): Ana umri wa miaka 35 ,Éric Davis (Beki): ana umri wa miaka 35. Aníbal Godoy (Kiungo): Nahodha wa timu mwenye umri wa miaka 36,na Cecilio Waterman Mshambuliaji tegemeo mwenye umri wa miaka 35. 

 

Kikosi cha kimesheheni kizazi cha dhahabu ambacho kimecheza pamoja kwa karibu muongo mmoja Alireza Beiranvand (Mlinda Lango): Kipa huyu maarufu ana umri wa miaka 33,Ehsan Hajsafi (Beki/Kiungo) ana umri wa miaka 36,Shojae Khalilzadeh Beki mwenye umri wa miaka 37,

  • Mehdi Taremi Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 33 na Alireza Jahanbakhsh Winga mwenye umri wa miaka 32.

 

  • Nyota wenye umri mkubwa zaidi kwa Timu ya Taifa ya Colombia ni David Ospina Golikipa mwenye umri wa miaka 37,Camilo Vargas Golikipa mwingine mwenye umri wa miaka 37,James Rodríguez Mchezaji bora wa Kombe la Dunia 2014, sasa ana umri wa miaka 34,Juan Cuadrado ana umri wa miaka 38 na Johan Mojica (Beki): Beki wa kushoto mwenye umri wa miaka 33.
pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet