Como ya Fabregas waikomoa Man United, wainyuka 4 - 1
Eric Buyanza
October 22, 2026
Share :
Hali ya Manchester United imezidi kuwa mbaya baada ya kuchapwa mabao 4- 1 na timu ya Como inayonolewa na nyota wa zamani wa Chelsea, Cesc Fabregas katika Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA Champions League).
Kipigo hicho kinaifanya Manchester United kujiweka katika mazingira magumu ya kufuzu hatua ya mtoano ambayo kwa sasa ligi hiyo inachezwa katika mfumo tofauti na zamani.






