pmbet

CRDB wadhamini wapya wa kombe la FA

Sisti Herman

April 2, 2024
Share :

Benki ya CRDB na imeingia mkataba wa udhamini na shirikisho la soka nchini TFF kwa miaka mitatu na nusu kwaajili ya kudhamini michuano ya kombe la Shirikisho la TFF (FA) ambapo CRDB itatoa shilingi Bilioni 3.76 kwa kipindi chote cha miaka mitatu na nusu.

“CRDB ndio anakuwa mdhamini wa kwanza wa kombe la Shirikisho” maneno ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia akizungumzia udhamini wa Benki ya CRDB kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.

“Sasa itaitwa CRDB Bank Federation Cup” maneno ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza kwenye hafla ya kuingia mkataba wa kudhamini michuano ya FA. Kwa msimu huu watatoa dola laki moja za kimarekani sawa na shilingi milioni 255, sasa Kombe la FA litaitwa CRDB BANK FEDERATION CUP.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet