pmbet

CRDB yajibu madai ya Yanga.

Joyce Shedrack

June 10, 2025
Share :

Benki ya CRDB ambaye ni mdhamini mkuu wa kombe la Shirikisho Tanzania imetoa taarifa kuhusu madai yaliyotolewa na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Ally Kamwe kuhusu deni lao la fedha walizotakiwa kupewa baada ya kuchukua ubingwa wa kombe hilo msimu uliopita. 

 

Benki hiyo imeweka wazi kuwa imekwisha tekeleza matakwa ya kimkataba waliyoingia na TFF kama sehemu ya makubaliano ya udhamini wa mashindano hayo.

“Tungependa kuufahamisha umma na wadau wote wa soka kuwa Benki ya CRDB ni taasisi yenye kuzingatia weledi, kanuni na taratibu na kwa msingi huo tayari Benki ilikwisha tekeleza kikamilifu wajibu wake wa kifedha kwa TFF kama sehemu ya makubaliano ya udhamini wa mashindano haya. Malipo yote ya msimu uliopita yalifanyika kwa TFF kwa mujibu wa mkataba baina ya Benki ya CRDB na TFF”.

“Benki ya CRDB inatambua kuwa mbali na mchezo wa soka kuunganisha jamii yetu na kutoa burudani, lakini pia mchezo huu ni ajira kwa vijana wengi, hivyo dhamira yetu ni kuendelea kushirikiana na TFF, vilabu na wadau wengine katika kukuza mchezo huu kwa maslahi mapana ya Taifa letu”.Imesema taarifa ya CRDB.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet