pmbet

Cristiano Ronaldo achomoa kushiriki Kombe la Dunia.

Joyce Shedrack

June 7, 2025
Share :

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ureno na klabu ya AL Nassr Cristiano Ronaldo ametangaza kuwa hatashiriki michuano ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu yanayotarajia kuanza juni 15 Nchini Marekani.

President Cristiano Ronaldo! CR7 told 'he would win' vote in Portugal if  Al-Nassr superstar swapped goalscoring for politics | Goal.com

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 40 amefunguka hayo baada ya kuibuka tetesi nyingi zinazomuhusisha kujiunga na timu zinazoshiriki michuano hiyo ili apate nafasi ya kucheza.

 

“Sitakuwa sehemu ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu pamoja na kwamba nimepokea mialiko mingi na ofa nyingi maamuzi yamekaribia kukamilika kwa upande wangu”Amesema Ronaldo.

 

Ronaldo alitajwa kujiunga na timu nyingi ambazo zipo kwenye michuano hiyo zikiwemo timu kutoka Bara la Afrika kama Wydad Casablanca ambayo ni miongoni mwa timu zinazoliwakilisha bara hilo huko Nchini Amerika kuanzia juni 15 hadi julai 13.

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet