pmbet

Cristiano Ronaldo aomboleza kifo cha Diogo Jota kwa uchungu.

Joyce Shedrack

July 3, 2025
Share :

Nahodha wa klabu ya Al Nassr na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameonesha masikitiko kufuatia kifo cha mshambuliaji mwenzake wa timu yake ya taifa na klabu ya Liverpool Diogo Jota pamoja na ndugu yake Andre Jota.

It doesn't make sense - Cristiano Ronaldo pays emotional tribute to Diogo  Jota
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Ronaldo ameandika ujumbe mzito wa kuomboleza vifo hivyo akieleza mshtuko na huzuni aliyonao kwa kuondokewa na wachezaji hao wawili .

"Haina maana yoyote. Sasa hivi tulikuwa pamoja kwenye Timu ya Taifa, sasa hivi mlikuwa mmefunga ndoa. Kwa familia yako, kwa mke wako na watoto, ninatuma salamu zangu za rambirambi na kuwatakia kila la kheri duniani. Najua utakuwa nao daima. R.I.P. Diogo na Andre, sote tutakukumbuka."Ameandika Ronaldo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet