CRISTIANO RONALDO: 'Saudi Pro League' ni Bora kuliko 'Ligue 1'
Eric Buyanza
January 20, 2024
Share :
Nahodha wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo amedai kuwa Ligi ya Saudia (Saudi Pro League) ni bora kuliko Ligi ya Ufaransa (Ligue 1).
Kwa mujibu wa Ronaldo, SPL ina ushindani zaidi kuliko Ligi ya Ufaransa kwa sasa.
Akiongea kwenye tuzo za Globe Soccer, fowadi huyo wa zamani wa Manchester United alisema:
"Kiukweli nadhani Saudi Pro League ni bora kwa sasa kuliko Ligi ya Ufaransa kwa mtazamo wangu. Kwenye Ligi ya Ufaransa wana timu mbili au tatu zenye kiwango kizuri...lakini kwa Saudia nadhani kuna ushindani mwingi zaidi" alisema Ronaldo.
“Wanaweza kusema wanachotaka. Haya ni maoni yangu tu. Lakini nadhani kwa sasa sisi [SPL] tuko bora kuliko ligi ya Ufaransa.”