Crystal Palace yapata mbadala wa Michael Olise kutoka Arsenal
Eric Buyanza
May 6, 2024
Share :
Klabu ya Crystal Palace inaripotiwa kutaka kumsajili winga Reiss Nelson wa Arsenal ikiwa Michael Olise ataondoka katika dirisha kubwa la usajili.
Inaelezwa kuwa 'The Gunners' wanaweza kumuuza mchezaji huyo licha ya kwamba alisaini mkataba mpya mwaka jana.
Nelson mwenye umri wa miaka 22 amekuwa kwenye kikosi cha Mikel Arteta kwa mwaka 3 lakini ameshindwa kuonyesha uwezo wake kila anapopewa nafasi.