pmbet

Cuba yasema iko tayari kupambana ikivamiwa na Marekani

Eric Buyanza

April 17, 2026
Share :

Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel amesema nchi yake iko tayari kupambana iwapo itahitajika kufanya hivyo, ingawa haitaki makabiliano ya kijeshi kutoka kwa Marekani.

 

Diaz-Canel ameyasema haya wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya watu kwa ajili ya kuadhimisha miaka 65 ya azimio la Mapinduzi ya Kisoshalisti ya Cuba.

 

Rais huyo ameyasema haya huku mivutano ikizidi kati ya nchi hiz ombili na mgogoro wa Cuba ukiendelea kuwa mbaya zaidi kutokana na vizuizi vya nishati vya Marekani.

Mapema wiki hii, utawala wa Trump ulisema kuwa unaweza kuigeukia Cuba mara tu vita dhidi ya iran vitakapofika mwisho.
 

Awali Trump alitishia kuwa ataivamia Cuba kama jeshi la Marekani lilivyofanya Januari huko Venezuela na kuzuia usafirishaji muhimu wa mafuta kutoka nchi hiyo ya kusini mwa Amerika.
 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet