Cunha kupimwa afya dili lake la kwenda United laiva
Eric Buyanza
May 28, 2025
Share :
Matheus Cunha anatazamiwa kufanyiwa vipimo vya afya baada ya ya Manchester United kukidhi masharti ya kipengele cha kuachiliwa kwa mbrazil huyo cha pauni milioni 62.5.
United na Wolves walikuwa kwenye mazungumzo kujadili muundo wa malipo, ambapo awali United walikuwa wakitaka kulipa kiasi hicho kwa miaka mitano jambo lilipingwa na Wolves na hatimae wakafikia makubaliano ya kulipa kwa awamu tatu katika miaka miwili.
Wolves sasa wameipa United ruhusa ya kuendelea na mambo mengine ili kukamilisha usajili huo.