D Voice atamani kumiliki lebo yake amsaini Dulla Makabila na Meja Kunta.
Joyce Shedrack
June 6, 2025
Share :
Staa wa muziki wa Bongo Fleva nchini aliyetambulika kupitia muziki wa Singeli hadi kusainiwa na lebo ya WCB Wasafi D Voice amewataja wasanii ambao anatamani akiwa na lebo yake ya singeli wawe wasanii wake akiwemo Dulla Makabila,Meja Kunta na Mdogo Sajenti.
Wakati alipokuwa kwenye mahojiano na moja ya chombo cha habari kwa ajili ya ziara yake ‘D Voice Tour’ ameeleza kuwa atawasaini wasanii kama Meja, Sajent na wengineo.
“Endapo nitafungua lebo ya Singeli nitamsaini, Kiwanda, Sele Minamba, Dakota mtu hatari, Stizo naye ni mtu hatari, Monta D, Dony blee ni mkali anatokea Mbagala, Sajenti nitamchukua kama Chino atanikubalia, Dulla Makabila, Meja na Dogo Elisha".Amesema D Voice.
Unafikiri hiyo ndoto ya D Voice inaweza kufanikiwa ?.