'Dada Poa' ashikilia Bunduki ya mlinzi kama dhamana, mpaka atakapolipwa chake
Eric Buyanza
January 16, 2024
Share :
Huko nchini Zimbabwe kijana anayefanya kazi ya ulinzi aliyefahamika kwa jina la Evidence Mangonono mwenye umri wa miaka 27, amenyang'anywa bunduki yake ya kazi na 'Dada Poa' baada ya kushindwa kumlipa kutokana na kwa huduma aliyopewa.
Inaelezwa kuwa Januari 7 akiwa ofisini kwake Mangonono alibugia dawa ya kuongeza nguvu za kiume na baada ya muda akatumia huduma ya 'Dada Poa' huyo aliyetambulika kwa jina la Choice...huku tukio hilo likifanyika kwa siri upande wa nyuma wa benki ambako Mangonono alikuwa akifanya kazi kama mlinzi.
Hata hivyo baada ya Mangonono kushindwa kumlipa Choce, mwanadada huyo alichukua bastola kama dhamana ya shughuli hiyo ambayo haijalipiwa.
Hali ilizidi kuwa tete baada ya bosi wa Mangonono kugundua kutokuwepo kwa bunduki ya mlinzi wake na kuamua kuripoti tukio hilo polisi.
Baada ya Mangonono kuona sakata hilo limeshakuwa gumu, ilimbdi kutafuta hela kwa hali yoyote ambapo alifanikiwa na kurudishiwa bastola...lakini alikuwa ameshachelwa kwasababu swala hilo lilikuwa limekwishafika kwenye vyombo vya dola ambapo aliburuzwa mahakamani na kufunguliwa mashataka.