Dada wa Kim Jong Un aichimba mkwara Korea Kusini
Eric Buyanza
July 8, 2024
Share :
Kim Yo Jong, Dada mwenye nguvu wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amesema mazoezi ya hivi karibuni ya kijeshi ya Korea Kusini karibu na mpaka kati ya mataifa hayo mawili ni uchochezi usio na sababu.
Alisema mazoezi hayo ni jaribio la Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, kuongeza kwa makusudi mvutano kwenye peninsula ya Korea ili kuhamisha mawazo ya wananchi kutokana mzozo wa kisiasa unaomkabili ndani ya nchi yake.
Kim akaonya kuwa iwapo watagundua kuwa Korea Kusini imefanya kitendo chochote kinachoashiria kutangaza vita, basi majeshi ya Korea Kaskazini yatatekeleza mara moja kazi na wajibu wake uliowekwa na Katiba yao.