pmbet

Dada wa Kim Jong Un aishambulia serikali Korea Kusini

Eric Buyanza

August 20, 2025
Share :

Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un aliye na ushawishi mkubwa, ameituhumu Korea Kusini kwa kile amekiita kuwa "tabia ya undumilakuwili".

Ameishambulia nchi hiyo jirani kwa hatua yake ya kufanya mazoezi ya kijeshi na Marekani huku ikijaribu kujifanya ina urafiki na Korea Kaskazini.

Kupitia taarifa yake iliyochapishwa na shirika la habari la Korea Kaskazini, Kim Yo Jong, amesema utawala wa Korea Kusini unatekeleza "sera za kuicheza shere" serikali ya mjini Pyongyang kupitia matamshi ya kirafiki wakati inashirikiana kwa karibu na Marekani, iliyo hasimu wa Korea Kaskazini.

Matamshi yake yanafuatia ahadi iliyotolewa hivi karibuni na rais mpya wa Korea Kusini,  Lee Jae Myung ambaye alisema anataka kurekebisha mahusiano kati ya Korea Mbili na kupunguza mivutano ya miaka mingi.

Hata hivyo Bibi Yong amesema mazoezi ya kijeshi yaliyoanza Jumatatu kati ya Korea Kusini na Marekani ni uthibitisho wa tabia ya kuwa sura mbili ya viongozi wa Korea Kusini.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet