Dada yake Lionel Messi apata ajali harusi yake yaahirishwa.
Joyce Shedrack
December 24, 2025
Share :
Dada wa Nahodha wa Argentina na klabu ya Inter Miami ya Marekani Lione Messi,María Sol Messi amepata ajali ya gari huko Miami mapema baada ya kupoteza udhibiti wa gari lake na kugonga ukuta.

Maria ambaye zimesalia siku chache kabla ya kufikia siku yake ya kufunga ndoa Januari 3 2026 hajapata majeraha makubwa sana akiripotiwa kuendelea vizuri huku familia ya Messi ikisafiri kwenda Rosario kutumia sikukuu pamoja na kumpa msaada katika kipindi hiki .
Kutokana na ajali hiyo familia ya Messi imeamua kuahirisha harusi hiyo ya Maria na mpenzi wake Julián Arellano mpaka hapo itakapotangazwa tena baada ya afya ya mrembo huyo kuwa sawa.





