Dah! Ronaldo amtolea uvivu mwandishi wa habari
Eric Buyanza
July 6, 2026
Share :

Katika hali ambayo haikutegemewa mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo, alimtolea uvivu mwandishi wa habari alipokuwa kwenye mkutano na waandishi kuelekea mechi yao dhidi ya Hispania.
Ronaldo alimnyooshea kidole mwandishi mmoja (ambaye anatajwa kuwa mwandishi wa Brazil, Marcelo Bechler) na kuomba apewe kipaza sauti kwa sababu anajua mwandishi huyo huwa hampendi.
CRISTIANO: "Mpe maiki yule jamaa aliye mbele yako, yule ambaye hanipendi. Nataka kuona kama ataniuliza swali zuri."
MWANDISHI: Cristiano, hujambo? Nafurahi kuzungumza nawe. Ningependa kukuuliza: ni jambo gani limekuwa gumu zaidi kwako kucheza kwenye Kombe la Dunia ukiwa na umri wa miaka 41?
CRISTIANO: Jambo gumu zaidi ni kuzungumza na baadhi yenu, hasa wale ambao hawanipendi. Na wewe ni mmoja wao. Najua hilo. Sisahau nyuso za watu.
Nahitaji kumuona mtu mara moja tu, na uso wake hubaki kwenye kumbukumbu yangu.
Baada ya hapo Ronaldo alicheka na kuendelea kueleza kuwa kucheza soka katika kiwango cha juu akiwa na umri wa miaka 41 kunahitaji kujitoa mhanga.





