pmbet

Dakika 10 za kila mechi Argentina kusimama kumpa heshima Messi.

Joyce Shedrack

September 3, 2026
Share :

Shirikisho la Soka la Argentina limetangaza kuwa mechi zote za ligi nchini humo zitasimamishwa katika dakika 10 za mwanzo mwishoni mwa wiki hii, ikiwa ni sehemu ya heshima kwa nyota wa soka Lionel Messi baada ya kutangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa.

Lionel Messi retires from international soccer after leading Argentina to  2026 FIFA World Cup final

Messi, mwenye umri wa miaka 39, amekuwa akivaa jezi namba 10 ya Argentina na ameacha historia kubwa katika timu hiyo ya taifa. Uamuzi wake wa kustaafu umeibua hisia miongoni mwa mashabiki wa soka nchini Argentina na duniani kote.

 

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Argentina, waamuzi watasimamisha mchezo katika dakika ya 10 ya kila mechi kwa ajili ya dakika moja ya makofi ya heshima kumuenzi Messi na mchango wake kwa timu ya taifa.

 

Messi ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika historia ya timu ya taifa ya Argentina, akiwa na jumla ya mechi 207.

 

Akiwa nahodha, Messi aliiongoza Argentina kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar, mafanikio yaliyokamilisha safari yake ya mafanikio makubwa akiwa na timu ya taifa.

 

Mechi yake ya mwisho kwa Argentina ilikuwa katika fainali ya Kombe la Dunia la 2026 dhidi ya Hispania, iliyochezwa mwezi Julai.

 

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Messi kutangaza kustaafu soka la kimataifa. Mwaka 2016, aliwahi kutangaza kustaafu kabla ya kubadili uamuzi wake na kurejea kuichezea Argentina.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet