pmbet

Daktari aburuzwa mahakamani kwa kuharibu uume wa mteja!

Eric Buyanza

April 10, 2024
Share :

Mwanamume mmoja wa Kiitaliano mwenye umri wa miaka 40 amemburuza daktari mahakamani baada upasuaji aliofanyiwa wa kuongeza ukubwa wa uume kumletea shida ya ukosefu wa nguvu za kiume. 

Mwanamume huyo kutoka mji wa Tuscany, alimlipa daktari $5,400 (sawa na milioni 14 za kibongo) kwa ajili ya operation ya kuongeza ukubwa wa uume wake, lakini baada ya mwezi mmoja aliishia kumpigia simu daktari yuleyule akimlalamikia kukosa kabisa nguvu za kiume na hivyo kushindwa kulimudu tendo. 

Akijitetea mahakamani Daktari huyo alidai kuwa baada ya upasuaji mteja wake aliridhika na matokeo ya upasuaji kwa kuweka saini kwenye kitabu maalum, na kuonyesha mahakamani hapo vielelezo vya uthibitisho huo. 

Hata hivyo, mahakama ilitupilia mbali madai yake, ikitoa uamuzi kwamba mgonjwa hakuwa na ufahamu wa hatari ambazo zingeweza kuja kumkabili kutokana na athari za upasuaji huo...na kuongeza kuwa ni kazi ya daktari kumhakikishia mteja huduma zisizo na shaka au kumtahadharisha mapema mteja kwamba lolote linaweza kutokea baada ya upasuaji. Mahakama ikahitimisha kwa kumtaka Daktari kumlipa fidia mlalamikaji ya $165,700 (sawa na milioni 427.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet