Daktari aenda jela kwa kubaka wagonjwa 229 wakiwamo watoto
Eric Buyanza
May 29, 2025
Share :
Mahakama ya Ufaransa imetoa kifungo cha miaka 20 jela kwa daktari bingwa wa upasuaji Joel Le Scouarnec, mwenye umri wa miaka 74 ambaye alikiri kuwanyanyasa kingono mamia ya wagonjwa, wengi wao wakiwa watoto, kwa zaidi ya miongo miwili.
Kesi hiyo iliyodumu kwa miezi mitatu ya, imefichua ukubwa wa uhalifu wake na mateso ya waathiriwa lakini pia imezua maswali kwa nini juhudi hazikufanyika mapema ili kumzuia.
Joel amekutwa na hatia ya kuwanyanyasa kingono na kuwabaka wagonjwa 229 katika kliniki yake mjini Vannes.
Hukumu ya miaka 20 jela kwa uhalifu mkubwa wa ubakaji iliyotolewa na hakimu mfawidhi Aude Buresi ndiyo ya juu zaidi ambayo inaweza kutolewa nchini Ufaransa kwa shtaka la ubakaji uliokithiri, ambapo hukumu hazijumuishwi pamoja kwa kila kosa alilofanya.