Daktari wa Azam Fc afariki dunia, kuzikwa kesho
Sisti Herman
February 28, 2024
Share :
Klabu ya Azam FC imetangaza kuwa Daktari wake Mwanandi Mwankemwa amefariki dunia leo jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.
“Kwa masikitiko makubwa tunapenda kutangaza kifo cha Daktari wetu, Dr. Mwanandi Mwankemwa, aliyefariki dunia kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, leo Jumanne jioni.” imesema Azam FC kupitia taarifa yake kwa umma.
Mazishi ya Dr. Mwankemwa yatafanyika siku ya Alhamis saa 7 mchana katika makaburi ya Kinondoni.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Mwanagati, Kitunda.
Marehemu Dr. Mwanandi amekuwa daktari wa michezo kwa zaidi ya miaka 40.