Daktari wa miaka 70 jela kwa kumbaka mwanamke Hospitali
Eric Buyanza
August 12, 2025
Share :
Mahakama Kuu ya Anuradhapura nchini Sri Lanka imemkuta na hatia daktari mwenye umri wa miaka 70 kwa kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 25, ambaye alikuwa amefika katika kituo cha matibabu ili kuondoa kitanzi cha uzazi ambacho kilikuwa kimepandikizwa mwilini mwake.
Hakimu aliamuru daktari huyo ahukumiwe kifungo cha miaka 15 jela na mlalamikaji alipwe fidia ya milioni moja na nusu.
Hakimu pia alimhukumu daktari kifungo cha miaka mitatu jela ikiwa atashindwa kulipa fidia hiyo.
BBC