"Damaro hata ipite miaka 100 hawezi kucheza Timu ya Taifa"Magori.
Joyce Shedrack
April 7, 2026
Share :
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Crescentius Magori amethibitisha kuwa wamethibitisha kuwa wataenda CAS na FIFA kwenye jambo la Uraia wa Mohamed Damaro.

“Mwaka jana na sisi tuliandika barua ya kubadili uraia wa wachezaji wetu lakini haijajibiwa hadi leo. Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa haipo kwenye mizania sawa sio japo sawa. Hili japo sio tu tunakwenda CAS lakini pia tunaiandikia FIFA".
"Kama mtu anapewa uraia ili tu achezee klabu pekee bila timu ya taifa ni jambo ambalo halikubaliki. Damaro hata ipite miaka 100 hawezi kucheza timu ya Taifa. Jambo lingine ambalo TFF walitakiwa walifanye, kama kanuni zetu halizungumzii hilo basi wangetumia kanuni za juu kufanya maamuzi.”Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Crescentius Magori.





