pmbet

Dangote atangazwa mtu tajiri zaidi Afrika kwa mwaka wa 13 mfululizo!

Eric Buyanza

January 26, 2024
Share :

Mfanyabiashara wa Nigeria Aliko Dangote ameorodheshwa na jarida la Forbes kama mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mwaka wa 13 mfululizo, licha ya matatizo ya kiuchumi nchini kwake.
 

Mabilionea 20 kwenye orodha hiyo wana thamani ya dola bilioni 82.4 kwa pamoja.
 

Utajiri wa Bw. Dangote umeongezeka kwa dola milioni 400 katika mwaka uliopita hadi kufikia thamani ya dola bilioni 13.9, kulingana na Forbes.

Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 66 alijitajirisha kwa saruji na sukari na mwaka jana alifungua kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lagos, kitovu cha uchumi cha Nigeria.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet