Dangote awekeza kwenye sekta ya Utalii nchini Kenya
Sisti Herman
February 6, 2026
Share :

Aliko Dangote, tajiri nambari moja barani Afrika, ameingia rasmi kwenye sekta ya utalii nchini Kenya kwa kununua kampuni ya Pollman’s Tours and Safaris
Makubaliano hayo, yaliyoidhinishwa na Mamlaka husika ya Kenya, na kusema hayatarajiwi kuathiri ushindani wa soko au ajira
Pollman’s, iliyoundwa miaka ya 1950, ni moja ya makampuni ya zamani zaidi ya utalii nchini Kenya, na umiliki mpya unalenga kukuza urithi wake na upanuzi wa huduma zake.
Kwenye uwekezaji huo tajiri huyo ameripotiwa kuwekeza $ 30 Millions (zaidi ya Tsh bil. 77)





