pmbet

Dani Alves mahakamani kwa ubakaji

Eric Buyanza

February 7, 2024
Share :

Mlinzi wa kulia aliyewahi kucheza Barcelona, Dani Alves amefikishwa mahakamani nchini Uhispania akituhumiwa kumbaka mwanamke kwenye kumbi moja ya starehe huko Barcelona katika tukio lililofanyika Desemba 2022.
 

Alves alikuwa chini ya ulinzi kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa bila dhamana.
 

Inaelezwa kuwa beki huyo wa Brazil huenda akatupwa lupango miaka 12 kama akipatikana na hatia. Hata hivyo Dani amekanusha kukutana na mwanamke huyo.
 

Zaidi ya watu 30 akiwemo Dani Alves na mke wake wa zamani wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.
 

Jumatano (leo) kesi hiyo itaendelea katika mahakama ya Barcelona, ​​huku Alves akitarajiwa kutoa maelezo yake ya mwisho baada ya kukana mashtaka yote dhidi yake.
 

Hukumu ya kesi hiyo itatolewa Februari 27, 2024.    
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet