Dante kama Bocco tu akabadhiwa timu ya vijana ya Bayern Munich.
Joyce Shedrack
June 2, 2026
Share :
Klabu ya Bayern Munich imetangaza kuwa beki wa zamani wa klabu hiyo, Dante atakuwa kocha mkuu wa Kikosi cha pili.

Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 42, anakwenda kuchukua nafasi ya Holger Seitz na inakuwa kazi yake ya kwanza ya uzoefu kama kocha.
Dante aliichezea Bayern kutoka 2012 hadi 2015, na kufanikiwa kucheza mechi 133 kwa timu hiyo ya mjini Munich, akifunga mabao 5 na kutoa asisti 8.





