Dar City yaanza kwa kishindo BAL
Sisti Herman
March 27, 2026
Share :

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa wa mpira wa Kikapu Afrika (BAL), Dar City imeanza kwa kishindo baada ya kuwafunga Johannesburg Giants vikapu 100 kwa 70.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Pretoria nchini Afrika kusini, mchezaji wa Dar City, Nisre Zouzoua raia wa Ivory Coast ameibuka nyota wa mchezo baada ya kufunga vikapu 35, rebound 5 na asisti 1.
Dar City itashuka tena dimbani kesho kucheza dhidi ya Nairobi City Thunder.





