Daraja laporomoka baada ya kugongwa na meli ya mizigo
Eric Buyanza
March 26, 2024
Share :
Daraja muhimu huko Baltimore, Maryland nchini Marekani limeanguka asubuhi ya leo baada ya kugongwa na meli kubwa iliyobeba shehena ya makontena.
Msemaji wa Idara ya Zimamoto ya Jiji la Baltimore alisema daraja hilo liliporomoka ndani ya mto Patapsco ambapo kwa taarifa za awali watu saba na magari kadhaa yameanguka ndani ya mto huo na operesheni ya uokoaji ilikuwa ikiendelea.