Davido afanya kufuru amzawadia mkewe saa ya Milioni 700.
Joyce Shedrack
August 11, 2025
Share :
Staa wa muziki wa Afrobit kutoka Nigeria David Adeleke maarufu Davido amemzawadia mke wake Chioma Adeleke saa ya mkononi aina ya Richard Mille RM037 yenye thamani ya dola 300,000 (takriban shilingi milioni 760) kama zawadi ya harusi.

Saa hiyo ni toleo la maalum lililotengenezwa kwa dhahabu ya white gold na kuwekewa almasi nyingi, ikionyesha hadhi na mapenzi makubwa kati ya wanandoa hao.