Davido agoma kugeuzwa kitega uchumi na mama wa mtoto wake
Joyce Shedrack
June 20, 2024
Share :
Msanii maarufu kutoka nchini Nigeria David Adeleke maarufu kama Davido amemfungulia mashataka mama mzazi wa binti yake wa kwanza mwanadada Sophia Momodu kwa kumtumia binti yao ili kujinufaisha kifedha kupitia malezi ya mtoto huyo anayeitwa Imade.
Wanasheria wa Davido, Olaniye Arije na Okey Barrah tarehe 17/06/2024 waliwasilisha hoja za msingi kwenye mahakama kuu ya mji wa Lagos,inayoiomba mahakama hiyo kumpa Baba wa mtoto haki ya malezi ya binti yake kwa kuondoa vikwazo vyovyote.
Davido amedai kuwa mzazi mwenzake mara kwa mara alikuwa akihitaji fedha nyingi na kukataa makubaliano aliyoyatoa, licha ya kutekeleza majukumu yake kwa Imade (Binti) kama Baba.
Katika kesi hiyo Davido ameeleza kuwa; "Sophia alikataa nyumba ya Naira milioni 200 (TZS mil. 350) yenye bwawa la kuogelea niliyonunua kwa ajili ya binti yangu Imade na yeye, lakini anataka niwe namlipia kodi ya Naira 5M (TZS mil. 9) kila mwaka, na pia alidai niwe namlipa mfanyakazi wake wa nyumbani dola 800 (TZS mil. 2.1) kwa mwezi na kutuma dola 19,800 (TZS milioni 51.6) kila mwaka kama pesa za matumizi."
Sambamba na hilo Davido amesema aliwahi kumnunulia mwanae gari aina ya Range Rover SUV kwa ajili ya usafiri wa mtoto kwenda shule lakini kuna siku akapigiwa simu kutoka shuleni kwa binti yake na kupewa taarifa za utoro wa mtoto alipomuuliza mzazi mwenzake kwanini mtoto haendi shule akajibu gari limeharibika hali iliyosababisha Davido kuongeza gari nyingine aina ya Highlander SUV na fedha kiasi cha Naira 5.8M zaidi ya Milioni 10 za kitanzania kwa ajili ya matengenezo ya gari.
Mahusiano ya wawili hao yalivujika miaka michache mbele baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyo mwaka 2015, na kukubaliana kushirikiana kwenye malezi ya mtoto.