Davido aibiwa hela siku ya harusi yake.
Eric Buyanza
July 3, 2024
Share :
Nyota wa muziki kutoka Nchini Nigeria David Adeleke maarufu kama Davido amehofia kuibiwa hela alizopewa kama zawadi siku ya harusi yake na mpenzi wake Chioma iliyofanyika jumanne ya Juni 25/6/2024 Lagos Nchini Nigeria.
Msanii huyo amechapisha video iliyoambatana na ujumbe wa kudhihirisha wasiwasi wake kupitia mitandao ya kijamii akisema kuwa pesa walizomwagiwa haziendani na uhalisia.
Davido amesema video zote za fedha walizomwagiwa kwenye harusi yake na Chioma haziendani na kile walichopeleka nyumbani kwao.