pmbet

Davido aijaza kwa mara nyingine O2 Arena

Eric Buyanza

January 19, 2024
Share :

Mkali wa Afrobeat toka Nigeria, Davido, kama kawaida yake ameujaza kwa mara nyingine tena uwanja wa ndani wa O2 Arena wa jijini London siku kadhaa kabla ya show yake aliyoipa jina la ‘Davido Invasion’ itakayofanyika Januari 28, 2024.
 

Tukisema ameujaza tunamaanisha (tayari tiketi zote za tamasha hilo zimeshanunuliwa).
 

Uwanja huo maarufu sana duniani una uwezo wa kuchukua watu elfu ishirini (20,000).
 

Ikumbukwe hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Davido kujaza Arena hiyo, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2019.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet