Davido aja na na mtandao wake wa kijamii
Sisti Herman
February 18, 2024
Share :
Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Davido, ameingia katika teknolojia ya kutengeneza mtandao wa kijamii ‘Chatter’ambapo utajihusisha na mwaliko maalum kwa ubunifu wa maudhui, kushiriki katika mawasiliano na mijadala kwa njia ya sauti na Video.
Mtandao huo unatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu kukiwa na lengo la kutoa uzoefu tofauti na mitandao mengine na kuleta ushindani kwa mitandao mengine kama X Spaces.