Davido akutana na Rais wa Ufaransa kujadili mipango ya maendeleo
Eric Buyanza
October 24, 2025
Share :
Kupitia ukurasa wa X, mkali wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria, Davido, amefichua madhumuni ya mkutano wake na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.
Kwa mujibu wa Davido, yeye na Macron walijadili maendeleo ya kimataifa kwa ujumla wake.
"Ilikuwa ni heshima kubwa kukutana @EmmanuelMacron na kushiriki maono yetu kwa ajili ya ulimwengu bora", aliandika Davido.
Davido aliandamana na meneja wake, Asa Asika.






