Davido amtaja msanii pekee wa Marekani atakayejisumbua kumuomba kolabo
Eric Buyanza
April 17, 2024
Share :
Nyota wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria, David Adeleke (Davido), amesema kwasasa ukimuacha Chris Brown, hawezi kujisumbua kuomba kolabo na msanii mwingine yoyote wa Marekani.
Davio aliongea hayo hivi majuzi kwenye 'Podcast' na Sway's Universe.
"Kando na Chris Brown, sitajisumbua kwa ushirikiano na msanii mwingine yoyote wa Marekani,” alisema.
Ikumbukwe Davido ameshawahi kufanya ngoma "Blow My Mind' akimshirikisha Chris Brown.