Davido atangaza siku ya kuacha muziki
Eric Buyanza
May 10, 2024
Share :
Kutoka Naigeria, nyota wa muziki wa Afrobeat, David Adeleke (Davido), amedokeza kuwa anatarajia kuacha muziki baada ya albamu yake inayofuata.
Davido anasema amefikia uamuzi huo baada ya kugundua kuna watu hawataki kabisa kumuona kwenye tasnia hiyo.
Katika siku za karibuni msanii huyo aliwahi kusema kwamba tangu aingie kwenye tasnia, wenzake wengi hawana amani.