pmbet

Davido atoa milioni 480 kusaidia yatima Nigeria

Eric Buyanza

February 21, 2024
Share :

Tumeona wasanii wengi wa nje na hata baadhi yao hapa Afrika waliopata mafanikio kupitia tasnia mbalimbali wakirudisha kwa jamii kupitia kipato chao.
 

Hayo yamedhihirishwa hapo jana kwa mwanamuziki wa AfroBeat kutoka nchini Nigeria, Davido kuahidi yeye na taasisi yake kutoa naira milioni 300 (sawa na shilingi milioni 480 za kibongo) kama mchango wake kwa mwaka huu kwenda kusaidia vituo vya watoto yatima wa Nigeia.
 

Kupitia ukurasa wake wa instagram mwanamuziki huyo aliandika...

“Mimi na taasisi yangu tunaahidi kutoa kiasi cha naira milioni 300, (sawa na shilingi milioni 480 za kibongo) kwa vituo vya watoto yatima kama mchango wangu wa mwaka kwa Taifa”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet