Davido azindua mtandao wake wa kijamii uitwao 'Chatter'
Eric Buyanza
July 12, 2024
Share :
Nyota wa muziki wa Afrobeats kutoka Nigeria, Davido, amezindua 'App' yake ya mtandao wa kijamii iitwayo Chatter.
Davido alitangaza uwepo wa 'App' hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii wa X (zamani Twitter) mapema leo Ijumaa.
Mwanamuziki huyo ameweka wazi kuwa anamiliki mtandao huo kwa ushirikiano na rafiki yake wa karibu aitwae Sir Banko.