pmbet

Davido kutoa ngoma mpya na Chris Brown.

Joyce Shedrack

March 28, 2025
Share :

Urafiki wa Davido na Chris Brown umekuwa wa faida kubwa kati yao tangu walipofahamiana na wawili hao wamezidi kuburudisha dunia kwa kutoa vichupa vikali , kwa awamu nyingine tena Davido amethibitisha kuwa yuko kwenye harakati za kumalizia kolabo ya pamoja na mwanamuziki nyota wa Marekani, Chris Brown.

Davido adai ana zaidi ya nyimbo 20 mpya na Chris Brown 'Yule anafanya kazi  kama mashine'

Davido ameyasema hayo kwenye Subaru World Stream kuwa collabo hiyo iko njiani na mashabiki wanaweza kutarajia kazi kubwa kutoka kwao.

Davido na Chris Brown nyimbo nyimbo yao ya kwanza kama Blow My Mind iliyotoka 2019 na Hmmmm ambayo bado mwezi mmoja ifikishe mwaka , ambazo zilipata umaarufu mkubwa duniani , hivyo huenda hii inayokuja ikawa ni kali kuliko zote zilizopita kutokana na wawili hao wakikutana hakuna jambo bovu.

Tarehe rasmi ya kuachia mradi huo mpya haijatajwa ila tangazo hili limeibua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Afrobeat na R&B.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet