Davido kuwekeza kwenye filamu, asema anaweza kuigiza
Eric Buyanza
April 19, 2025
Share :
Kutoka Nigeria, staa kunako muziki wa Afrobeats, David Adeleke (Davido), amesema mwaka huu ataingiza pesa kwenye tasnia ya filamu nchini humo.
"Ninawekeza katika filamu kadhaa mwaka huu, kiwanda cha filamu kwa sasa barani Afrika ni kama kinafilisika. Kwa hivyo, hakika tutaingia kwenye eneo hilo.
"Pia naweza kuigiza, kweli naweza kuigiza . huwa ninaigiza kwenye video zangu za muziki...na niliigiza katika video za muziki kama vile 'Jowo' na 'Nwa Baby'."" alisema Davido