Dawa 5 zinazopunguza nguvu za kiume na hutumiwa sana
Eric Buyanza
June 22, 2026
Share :
Tafiti mbalimbali zimegundua dawa ambazo zina athari kubwa juu ya nguvu za kiume na hutumiwa mara kwa mara.
Hapa chini ni dawa zinazopaswa kuepukwa na wanaume, ili wasipoteze nguvu zao za kiume.
Maisha ya kitandani ni moja ya mahitaji makubwa ya mwanadamu, lakini wakati mwingine huja na changamoto.
Sababu mbalimbali zinaweza kusababisha vikwazo hivi, lakini baadhi ya sababu zinahusishwa na aina tano ya dawa kama ilivyotangazwa na Shirika la Habari la ANI na kunukuliwa na BBC, ambalo mwaka 2022 ilitayarisha taarifa maalum juu ya mada hii.
DAWA YA KUTULIZA MAUMIVU
Watu wengi hawasiti kutumia dawa za kutuliza maumivu hata kwa maumivu wanayohisi ni madogo.
Lakini, je, unajua kwamba dawa zilezile za kutuliza maumivu zinaathiri uanaume wako na kuufanya usiwe na matokeo mazuri kitandani?
Dawa za kutuliza maumivu huzuia kuundwa kwa seli za uzazi na huvuruga homoni nyingi ambazo ni muhimu katika kufanya tendo la ndoa kati ya wanaume na wanawake.
DAWA YA KUZUIA WASIWASI (ANTI-ANXIETY)
Watu wengi wanaolalamika kuhusu matatizo ya akili na kuwa na wasiwasi hutumia dawa ili kukabiliana na hofu.
Walakini, dawa kama hizo hupunguza hamu ya tendo la ndoa.
DAWA ZA MSONGO WA MAWAZO (SONONA)
Dawa hizi, zinazojulikana kama "benzodiazepines," mara nyingi hutumiwa kutibu magonjwa ya wasiwasi, kama vile wakati mtu anaogopa vitu ambavyo havipo na yuko peke yake.
Magonjwa mengine ambayo hutumia dawa hizi ni pamoja na kukosa usingizi na maumivu ya misuli.
Lakini, upande wa madhara ni kwamba huathiri utendaji wa seli za uzazi wa kiume na hisia.
DAWA YA KUZUIA SHINIKIZO LA DAMU
Wagonjwa wanaotumia dawa za shinikizo la damu wanaweza pia kukumbana na changamoto nyingine ambayo ni kupungua kwa nguvu zao.
Dawa hizi zinaingiliana moja kwa moja na mishipa ya damu na pia hufanya kazi na mfumo wa neva.
DAWA ZA KIFUA KIKUU
Dawa za dukani kama vile dawa za kupuliza katika pua zilizoziba na dawa za kawaida za kupunguza kuziba kwa pua zina athari zake.
zinaweza kusababisha matatizo katika tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake.
BBC





