pmbet

DC Mtatiro afungia Kanisa linalowakataza Waumini kujifungua Kituo cha Afya

Sisti Herman

June 30, 2024
Share :

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, amelifunga Kanisa la ‘Church of God’ lililopo kijiji cha Mendo, Tarafa ya Itwangi, Wilaya ya Shinyanga ili kupisha uchunguzi maalum huku Mchungaji wa Kanisa hilo na wenzake wakihojiwa na watafikishwa Mahakamani kwa kosa la kuwashawishi Waumini kutoenda kliniki wakiwa Wajawazito na kuwashawishi pia wajifungulie Kanisani ambapo Mtatiro amesema hawezi kusubiri matukio mabaya kama ya Kibwetere (Uganda) au Shakahola (Kenya), yatokee Shinyanga.

Akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wakili Mtatiro amelifunga Kanisa hilo baada ya tukio la June 17, 2024 ambapo mmoja wa Waumini wa Kanisa hilo mwenye umri wa miaka 24 alishawishiwa na Mchungaji wa Kanisa hilo akajifungulie Kanisani badala ya kwenda kliniki “Aliposhikwa na uchungu, Wazazi wakamchukulia usafiri aelekee kliniki, akakataa katakata, akakimbilia kwa Mchungaji, wakaanza maombi, wakamzalisha kwa kuvuta kichanga kama vile unavyovuta kamba kwenye mashindano, kikatoka kikiwa kimefariki baada ya kichwa kushindwa kutoka kwa muda mrefu, Madaktari waliwahi eneo la tukio na kuokoa maisha ya Muumini huyo”

“Kwa mujibu wa Wananchi Mchungaji huyo anawahamasisha Watu wasiende kliniki wanapokuwa Wajawazito, badala yake wakachukue huduma za Kliniki kwake, pia wanapokaribia kujifungua wasiende kliniki na badala yake wakajifungulie Kanisani kwake na anahamasisha Waumini wasiwapeleke kliniki Watoto wa miaka 1 - 5 na pia Mchungaji huyo anawakataza katakata Waumini wake wasitoe majina ya ukoo kwa watoto wao, majina kama Masanja, Ng’wana Mabula na mengine kwake ni mwiko Waumini nao wametii”

“Mwaka jana aliwatia Waumini hasara kubwa, aliwakataza kulima mazao yoyote katika mvua za November na December 2023 kwa maelekezo kuwa mvua hizo ni za laana na Mungu amemuotesha, akawataka watumie mvua za January - March 2024, Waumini waliofuata maelekezo yake wameambulia patupu, waliolima kwa mvua alizoita za laana za Nov na Dec 2024, wamevuna hasa”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet