pmbet

De Bruyne bado yupo sana Man City.

Joyce Shedrack

July 23, 2024
Share :

Kocha Mkuu wa mabingwa wa ligi Kuu Uingereza Man City,Pep Guardiola amethibisha kuwa  kiungo wake Kevin De Bruyne  hataondoka ndani ya kikosi cha timu hiyo katika dirisha hili la usajili.

Guardiola amekanusha taarifa hizo zilizokuwa zinasambaa sehemu mbalimbali kuwa nyota huyo huwenda akaondoka nchini Uingereza kutokana na kupata ofa nono nchini Saudi Rabia.

 

Meneja huyo amesema “Kevin haondoki Man City” wakati akiongea na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Celtic .

 

Guardiola aliongeza kama kuna mchezaji yoyote ataondoka wataweka wazi lakini ana asilimia kubwa ya kuwa na kikosi chake chote alichokuwa nacho msimu unaokuja.

 

De Bruyne alihusishwa kutimkia Nchini Saudia Arabia ambapo taarifa zilikuwa zinasema tayari kuna timu zilimtengea kiasi kikubwa cha fedha ili kunasa saini ya kiungo huyo ambaye bado anamkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ya sasa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet