De Bruyne na rekodi mpya City
Sisti Herman
April 7, 2024
Share :
Mara baada ya jana kufunga mabao mawili kati ya manne waliyoshinda dhidi ya Crystal Palace, kiungo mshambuliaji wa klabu ya Man City na timu ya Taifa ya Ubelgiji Kelvin De Bruyne rasmi sasa ameingia kwenye orodha ya wachezaji waliofikisha mabao 100 kwenye klabu hiyo.
De Bruyne amefikia rekodi hiyo baada ya mechi 372 akiwa na uzi wa City huku akifikisha asisti 167 baada ya jana hiyo hiyo pia kupika bao safi kwa Erling Halland.
Kwenye mchezo huo City ambao City waliwafunga Palace mabao 4-2, magoli mengine ya City yamefungwa na Erling Halland na Rico Lewis.