De Gea anukia Newcastle
Eric Buyanza
December 5, 2023
Share :
Newcastle United inaweza kumsajili kipa wa zamani wa Manchester United, David de Gea ili kuchukua nafasi ya Nick Pope ambaye amepata majeraha ya bega na anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi minne.
Pope aliumia Desemba 2, 2023 wakati Newcastle ikipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Man. United, katika Premier League
De Gea ni mchezaji huru kwa sasa, mara ya mwisho mshahara wake ulikuwa Pauni 375,000 (Tsh. Bilioni 1.1) kwa wiki, kama Newcastle ikimsajili inaelezwa atalazimika kukubali kulipwa chini ya kiwango hicho.