Deal Done...! Clatous Chama ni mali ya Yanga.
Joyce Shedrack
July 1, 2024
Share :
Rasmi klabu ya Yanga SC imemtambulisha aliyekuwa kiungo Mshambuliaji wa Simba SC raia wa Zambia, Clatous Chama (33) kuwa mchezaji wao baada ya kumaliza mkataba wake na Simba Sc.
Chama alijiunga na Simba akitokea Lusaka Power Dynamos ya Zambia mwaka 2018 na kusaini mkataba wa miaka miwili, mwaka 2019 Chama aliongeza mkataba wa miaka 2 hadi mwaka 2022 kabla ya kutimkia Morocco katika klabu ya RS Berkane ya kwa mkataba wa miaka mitatu. Baada ya kuitumikia Berkane kwa muda mchache na baadae alirejea katika klabu yake ya awali Simba.
Tripple C amemaliza mkataba wake jana juni 30 na klabu yake iliyomleta Tanzania na leo julai 1 ametambulishwa na mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara kuwatumikia kwa mkataba wa mwaka mmoja.