DEAL DONE: João Gomes asajiliwa Aston Villa kwa pauni milioni 35
Eric Buyanza
July 20, 2026
Share :
Klabu ya Aston Villa F.C. imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Brazil, João Gomes, kutoka klabu ya Wolves kwa makubaliano ya ada ya pauni milioni 35.
Gomes amesaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo baada ya Wolves kushuka daraja msimu uliopita.
Usajili wake umekuja kama mbadala muhimu wa kuziba pengo la Youri Tielemans aliyehamia Manchester United pamoja na Amadou Onana aliyepata jeraha la goti.






